PURPOSE OF THE SERVICE CHARTER

The purpose of this Service Delivery Charter is to define the service standards expected from the Salaries and Remuneration Commission (SRC). SRC is committed to providing quality services that meet stakeholders’ needs, and further endeavours to attend to stakeholders with integrity, objectivity, confidentiality and competence.

OUR VISION

A productive public service that is fairly remunerated

OUR MISSION

To set, review and advise on equitable, competitive and fiscally sustainable remuneration and benefits in the public sector through research and analysis.

OUR CORE VALUES

The Commission commits to the following set of core values in service delivery:

  1. Fairness: We endeavour to be honest, fair and objective in all the Commission’s activities and decision-making.
  2. Accountability: We shall be accountable for our decisions or actions.
  3. Collaboration: We believe in the power of working together with stakeholders. We shall build, support and encourage collaboration across teams, organisations and sectors in order to achieve our mission.
  4. Integrity: We value high standards of ethical behaviour at all times. We shall uphold honesty and strong moral principles in all the Commission’s activities and decision-making.
  5. Innovation: We are committed to fostering an enabling environment that encourages continuous learning and relentless pursuit of creative solutions to achieve efficiency and effectiveness in service delivery.
  6. Transparency: We are committed to promoting transparency in our work. We shall be open in accordance with the law.

OUR MANDATE

  1. Set and regularly review the remuneration and benefits of all State officers; and
  2. Advice the national and county governments on the remuneration and benefits of all other public officers.

OUR ROLE

Section 11, of the Salaries and Remuneration Commission Act, 2011, provides that the Commission shall perform the following roles:

  1. Inquire into and advise on the salaries and remuneration to be paid out of public funds.
  2. Keep under review all matters relating to the salaries and remuneration of public officers.
  3. Advise the national and county governments on the harmonization, equity and fairness of remuneration for the attraction and retention of requisite skills in the public sector.
  4. Conduct comparative surveys on the labour markets and trends in remuneration to determine the monetary worth of the jobs of public officers.
  5. Determine the cycle of salaries and remuneration review upon which parliament may allocate adequate funds for implementation.
  6. Make recommendations on matters relating to the salary and remuneration of a particular State or public officer.
  7. Make recommendations on the review of pensions payable to holders of public offices.

OUR STAKEHOLDERS

The Commission’s stakeholders are broadly categorised as follows:

National Government Public
County Governments (Governors, Council of Governors Committees, Speakers, County Executive Committees, County Assemblies, County Public Service Boards, and County Assembly Service Boards) Civil Societies Organisations, Non-Governmental Organisations, Community-Based Organisations, Faith-Based Organisations
Parliament and Senate Employer organisations
Judiciary Private sector
Constitution Commissions and Independent Offices Professional bodies
Disciplined and uniformed services Pension schemes
Universities, research and tertiary institutions Opinion leaders
State corporations Development partners
Trade unions Diplomatic community
Media United Nations agencies

OUR COMMITMENT TO SERVICE DELIVERY

The Commission is committed to the provision of services in a fair, transparent, accountable, timely, effective and efficient manner.

  Service SRC’s Obligation Stakeholder’s Obligation Timeline
1.        Setting remuneration and benefits of State officers Set and publish a remuneration and benefit structure Provide required information during job evaluation and salary surveys Every four years
Issue advice on remuneration and benefits of a specific State officer Request for Commission’s advice on State officer’s remuneration and benefits Within 30 calendar days
2.        Advise on remuneration for Public officers Issue advisory communication on reviewed remuneration and benefits of other public officers Provide required information during job evaluation and salary surveys Every four years
Analyse requests for reviews and provide advice Submit request for advice on remuneration to the Commission Within 30 working days
3.        Conduct job evaluation for public sector Issue job grading structure for public sector institutions Provide required information Every four years (as per regulations)
Review of job evaluation results Evaluate request for review of job evaluation results from institutions as per Commission’s guidelines Submit request for review in accordance with Commission’s guidelines Within 51 working days
4.        Issue advice on Collective Bargaining Negotiations (CBN) Review CBN requests from institutions and provide advice Submit request for advice on a CBN, in accordance with Commission’s CBN guidelines Within 30 calendar days
Issue a clearance letter to facilitate registration of Collective Bargaining Agreement (CBA) Conclude CBN within parameters advised by the Commission Within 5 working days from receipt of signed CBA.
5.        Communication of Commission’s existing decisions Deliberate on requests for advice from institutions Request for Commission’s advice and submit the required information Within 7 working days after Commission’s decision
6.        Provision of information about the Commission Avail requested information Request for information Within 24 hours
Upload Circulars and other Commission’s communication onto SRC’s website and social media platforms. Visit SRC’s website and social media platforms Within 24 hours
7.        Provision of information to the media Respond to specific media requests, queries and enquiries Request for information through the SRC’s website, social media platforms, email or phone Within 24 hours
Share press releases, press statements, hold press conferences/briefings As per the specific need
8.        Publishing tenders, quotation documents Prepare and publish the tenders, quotations documents Check tenders on SRC’s website, media, social media or quotations in emails, and respond on time Within 2 working days
9.        Payment for procured goods, services or works Ensure the goods, services and works are within the Commission’s specifications Deliver goods/services as per Commission’s order Within 60 calendar days after the delivery
10.    Providing input to legislative proposals touching on SRC’s mandate Reviewing legislative proposals and providing input thereon Providing information on the legislative proposals As per the request
11.    Undertaking capacity building and sensitisation on SRC’s advisories Capacity building and sensitisation undertaken Attendance to the sensitisation meetings As per the request
12.   Provision of required statutory information to government agencies Submit the required information. Receive and process the submitted information As stipulated
13.   Stakeholders’ sensitisation, advocacy and awareness Timely response to feedback from stakeholders Send feedback through the SRC’s website, social media platforms, email, phone or physically visiting the office As per the specific need

Note: All our services are free of charge.

HAVE YOUR SAY

The Commission aims to provide quality services to all stakeholders. The Commission is open to receiving complaints, suggestions and comments to improve its service delivery. Any compliment or any service rendered that does not conform to the above standards, or any officer that does not live up to the commitment to courtesy and excellence in service delivery, should be communicated.

When you contact us due to a compliments, suggestions, comments or complaints, please explain your concerns clearly, indicate your full name, address and telephone number, and we shall respond to you within two working days.

Send your queries in-person, by phone, through our website, letter or email to:

Commission Secretary/Chief Executive Officer

Salaries and Remuneration Commission

Tel: +254 (20) 2710065/81

Email: info@src.go.ke

REVIEW OF THE CHARTER

This Service Delivery Charter shall be reviewed annually or as need arises.

WHERE WE ARE FOUND WORKING HOURS
Williamson House, 6th Floor, 4th Ngong Avenue

P.O. Box 43126, GPO-00100, Nairobi, Kenya

Tel: +254 (20) 2710065/81

Email: info@src.go.ke

Website: www.src.go.ke

 

SRC Social Media Platforms:

Twitter: @srckenya

Instagram: @srckenya

Flickr: srckenya

Facebook: Salaries and Remuneration Commission

LinkedIn: Salaries and Remuneration Commission

YouTube: Salaries and Remuneration Commission

Monday to Friday

8:00am to 1:00pm

2:00pm to 5:00pm

Excluding Public Holidays and Weekends

 

 

MKATABA WA UTOAJI HUDUMA
Tume ya Mishahara na Marupurupu

LENGO LA MKATABA
Lengo la Mkataba wa Utoaji Huduma ni kueleza kanuni za utendakazi wa Tume ya Mishahara na
Marupurupu. Tume imejitolea kutoa huduma bora zinazotimiza mahitaji ya wadau. Isitoshe, inafanya
kila jitihada kuwahudumia wadau kwa uadilifu, uaminifu, ustadi na bila mapendeleo.

MAONO
Kukuza sekta ya watumishi wa umma wanaopokea malipo ya sawa.

WITO
Kuweka kiwango, kutathmini upya na kushauri kuhusu mishahara na marupurupu yenye usawa,
yanayoridhisha na nafuu kwa sekta ya umma kupitia utafiti na uchanganuzi.

MAADILI YETU
Tume imejitolea kutekeleza maadili yafuatayo katika utoaji huduma zake:
a) Haki: Tunajizatiti kuwa waaminifu na wenye kutenda haki bila mapendeleo katika shughuli na
maamuzi yote ya Tume.
b) Uwajibikaji: Tutawajibikia maamuzi na matendo yetu.
c) Ushirikiano: Tunaamini katika kufanya kazi pamoja na wadau. Tutakuza, tutaunga mkono na
kuhimiza ushirikiano wa makundi, mashirika na sekta ili kutimiza malengo yetu.
d) Uadilifu: Tunathamini sana maadili ya kiwango cha juu wakati wote. Tutajifanya kila jitihada
kudumisha uaminifu na maadili thabiti katika shughuli na maamuzi yote ya Tume.
e) Ubunifu: Tumejitolea kukuza mazingira yanayotoa fursa ya kujiimarisha kimafunzo kila wakati
na kubuni mbinu zitakazoimarisha utoaji huduma bora na mwafaka.
f) Uwazi: Tunajizatiti kukuza uwazi katika kazi zetu. Tutakuwa radhi kupigwa darubini kuambatana
na kanuni za kisheria.

WAJIBU WETU
a) Kuweka kiwango na kutathmini upya mara kwa mara malipo ya Maafisa wote wa Serikali; na
b) Kushauri serikali ya kitaifa na za kaunti kuhusu malipo yanayowafaa watumishi wengine wote wa
umma.

JUKUMU LETU
Ibara 11 ya Sheria ya Tume ya Mishahara na Marupurupu, 2011, inaeleza kwamba Tume itatekeleza
majukumu yafuatayo:
a) Kuchambua na kushauri kuhusu kiwango cha mishahara na marupurupu kinachofaa kulipwa kutoka mfuko wa umma.
b) Kutathmini mara kwa mara masuala yanayohusu mishahara na marupurupu ya maafisa wa umma.
c) Kushauri serikali ya kitaifa na za kaunti jinsi ya kuwa na malipo yaliyo laini, sawa na kuridhisha ili
kuvutia na kudumisha wafanyakazi wa umma walio na ujuzi.
d) Kuandaa tafiti mbalimbali kuhusu sekta ya leba na mitindo ya ulipaji mishahara ili kubaini kiwango
cha malipo kinachostahili maafisa wa umma.
e) Kubaini nyakati za kuongeza mishahara na marupurupu ili Bunge liweze kutenga fedha za kutosha kutekeleza nyongeza hizo.
f) Kutoa mapendekezo kuhusu mshahara na marupurupu ya afisa mahususi wa Serikali au umma.
g) Kutoa mapendekezo kuhusu nyongeza ya malipo ya uzeeni kwa wanaohudumu katika ofisi za
umma.

WADAU WETU
Wadau mbalimbali wanaohusika na Tume ni kama wafuatavyo:

Serikali ya Kitaifa Umma
Serikali za Kaunti (Magavana, Kamati za Baraza la Magavana,
Maspika, Kamati za Wizara za Kaunti, Mabunge ya Kaunti, Bodi
za Kaunti za Kuajiri Watumishi wa Umma, na Bodi za Kuajiri
Wafanyakazi wa Bunge la Kaunti)
Mashirika ya Kiraia, Mashirika Yasiyo ya Serikali,
Mashirika ya Kijamii, Mashirika ya Kidini
Bunge na Seneti Waajiri
Idara ya Mahakama Sekta ya kibinafsi
Tume za Kikatiba na Ofisi Huru Vyama vya wataalamu
Vikosi vya ulinzi na usalama Hazina za uzeeni
Taasisi za vyuo vikuu, elimu ya juu na utafiti Viongozi wenye ushawishi
Mashirika ya Serikali Wafadhili
Vyama vya wafanyakazi Mabalozi na wanadiplomasia
Vyombo vya habari Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN)

AHADI YETU

Tume imejitolea kuhakikisha inatoa huduma kwa njia ya haki, uwazi, uwajibikaji, kwa njia mwafaka, utendakazi bora na kwa wakati.

  Huduma Wajibu wa SRC Jukumu la Mshikadau Muda
1.        Kuweka kiwango cha mishahara na marupurupu ya Maafisa wa Serikali Kuandaa mpangilio wa viwango vya mishahara na marupurupu Kutoa habari zinazohitajika wakati wa utafiti Kila miaka minne
Kupendekeza kiwango cha malipo ya Afisa mahususi wa Serikali Kuomba ushauri wa Tume kuhusu kiwango cha mishahara na marupurupu ya Afisa wa Serikali Katika siku 30 za kalenda
2.        Kupendekeza kiwango cha malipo ya Maafisa wa Umma Kutoa tangazo kuhusu nyongeza ya mishahara na marupurupu ya maafisa wengine wa umma Kutoa habari zinazohitajika wakati wa utafiti Kila miaka minne
Kuchambua maombi ya nyongeza ya malipo na kutoa ushauri Kuwasilisha barua ya kuomba ushauri wa Tume kuhusu kiwango cha malipo Katika siku 30 za kazi
3.        Kufanya tathmini ya kazi za sekta ya umma Kuandaa mpangilio wa madaraja ya mishahara kwa taasisi za sekta ya umma Toa habari zinazohitajika Kila miaka minne (kuambatana na kanuni)
Kuchambua matokeo ya tathmini ya kazi Kutathmini maombi ya kuchambua ripoti za tathmini za kazi za taasisi mbalimbali, kuambatana na kanuni za Tume Wasilisha barua ya kutaka tathmini kuambatana na kanuni za Tume Katika siku 51 za kazi
4.        Kutoa ushauri kuhusu Makubaliano ya Mishahara (CBN) Kuchambua maombi ya kutathmini CBNs za taasisi mbalimbali na kutoa ushauri Wasilisha barua ya kuomba ushauri kuhusu CBN, kuambatana na kanuni za Tume kuhusu CBN Katika siku 30 za kalenda
Kutoa barua ya kuidhinisha utambuzi na usajili mahakamani wa Mkataba wa Makubaliano ya Malipo (CBA) Kamilisha CBN kuambatana na mwongozo ulioshauriwa na Tume Katika siku 5 za kazi tangu kupokea CBA iliyotiwa saini
5.        Kuwasilisha maamuzi ya sasa ya Tume Kutathmini maombi ya taasisi mbalimbali zinazosaka ushauri Kuomba ushauri wa Tume na kutoa habari zinazohitajika Katika siku 7 za kazi baada ya uamuzi wa Tume
6.        Kutoa habari kuhusu Tume Wasilisha habari zilizoombwa Wasilisha ombi la habari Katika saa 24
Pakia Barua na notisi zingine za SRC kwenye tovuti ya Tume na kurasa za mitandao ya kijamii Tembelea tovuti ya SRC na mitandao yake ya kijamii Katika saa 24
7.        Kutoa habari kwa vyombo vya habari Jibu maombi mahususi ya vyombo vya habari, hoja na maswali Tuma maombi ya kupata habari kupitia tovuti ya SRC, mitandao yake ya kijamii, barua pepe ama simu Katika saa 24
Shiriki taarifa kwa vyombo vya habari, andaa mikutano/maelezo mafupi na waandishi wa habari Kulingana na kila hitaji
8.        Kuchapisha tenda, stakabadhi za ununuzi Andaa na chapisha zabuni, stakabadhi za ununuzi Angalia zabuni kwenye votuvi ya SRC, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii ama stakabadhi za ununuzi kwenye barua pepe, na kujibu kwa wakati Katika siku 2 za kazi
9.        Kulipia bidhaa, huduma ama kazi Hakikisha bidhaa, huduma na kazi zinatimiza matakwa ya Tume Wasilisha bidhaa/huduma kuambatana na oda ya Tume Katika siku 60 za kalenda baada ya kuwasilishwa
10.    Kuchangia mapendekezo ya kisheria yanayohusu majukumu ya SRC Kuhakiki mapendekezo ya kisheria na kutoa michango Kutoa maelezo kuhusu mapendekezo ya kisheria Kulingana na ombi
11.    Kukuza hamasisho kuhusu mapendekezo ya SRC Kufanya hamasisho Kuhudhuria mikutano ya hamasisho Kulingana na ombi
12.  Kutoa habari zinazohitajika kwa mashirika ya serikali Wasilisha habari zinazohitajika Kupokea na kutayarisha habari zilizowasilishwa Kama ilivyoelezwa
13.
Kuendesha hamasisho na kukuza ufahamu na uungwaji mkono miongoni mwa wadau Kujibu kwa wakati maoni ya wadau Kutoa maoni kupitia tovuti ya SRC, mitandao ya kijamii, barua pepe, simu ama kufika moja kwa moja ofisini Kulingana na hitaji

 

Fahamu: Huduma zetu zote zinatolewa bila malipo.

TOA MAONI YAKO

Tume inajizatiti kutoa huduma bora kwa washikadau wote. Tume iko wazi kupoikea malalamishi, mapendekezo na maoni jinsi ya kuimarisha huduma zake. Pongezi zozote na pia maoni kuhusu huduma zozote ambazo hazifikii viwango vya ubora viliyoelezwa hapo juu, ama afisa yeyote ambaye hazingatii uungwana na ustadi katika utendakazi wake, yanakaribishwa.

Unapowasilisha pongezi, mapendekezo, maoni ama malalamishi, tafadhali eleza hoja zako vizuri kisha utupe jina lako kamili, anwani na nambari ya simu, na tutawasiliana nawe katika muda usiozidi siku mbili za kazi.

 

Toa maoni yako moja kwa moja, kwa njia ya simu, kupitia tovuti yetu, barua ama barua pepe kwa:

 

Katibu wa Tume/Afisa Mkuu Mtendaji

Tume ya Mishahara na Marupurupu

Simu: +254 (20) 2710065/81

Barua pepe: info@src.go.ke

KUREKEBISHA MKATABA

Mkabata huu wa Utoaji Huduma utafanyiwa marekebisho kila mwaka ama inapohitajika

TUNAPATIKANA SAA ZA KAZI
Jumba la Williamson House, Orofa ya 6, Barabara ya 4th Ngong Avenue

S.L.P 43126, GPO-00100, Nairobi, Kenya

Simu: +254 (20) 2710065/81

Barua pepe: info@src.go.ke

Tovuti: www.src.go.ke

 

SRC pia tunapatikana katika mtandao ya kijamii:

·         Twitter: @srckenya

·         Instagram: @srckenya

·         Flickr: srckenya

·         Facebook: Salaries and Remuneration Commission

·         LinkedIn: Salaries and Remuneration Commission

·         YouTube: Salaries and Remuneration Commission

Jumatatu hadi Ijumaa

Saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana

Saa nane mchana hadi saa kumi na moja jioni

Isipokuwa Wikendi na Sikukuu za Umma

 



Skip to content